Saturday, March 9, 2013

UFARANSA YACHUKIZWA NA KITENDO CHA MASHOGA KUBAGULIWA.

BAADHI ya wanaharakati nchini Ufaransa wamechukizwa na kitendo cha Ligi ya Kulipwa ya Wanawake nchini Nigeria-NWPL kutoruhusu wachezaji wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kushiriki katika ligi hiyo. Barua ya wazi iliyoandikwa kwenda kwa balozi wa Nigeria nchini Ufaransa Akin Fayomi kutoka kwa wadau mbalimbali wa michezo na viongozi wa haki za raia nchini humo, ililaani mpango huo wa NWPL. Barua hiyo ilidai uamuzi uliochukuliwa na rais wa NWPL Dilichukwu Onyedinma hauelezeki kwani unakiuka haki za binadamu. Wanaharakati hao wanadai kitendo hicho hakiwezi kuvumilika na kama NWPL wakishindwa kutengua uamuzi wao huo wataliandikia barua Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kuingilia kati suala hilo.

No comments:

Post a Comment