Saturday, March 9, 2013
MONTPELLIER WAMNYATIA MARADONA.
RAIS wa klabu ya Montpellier ya Ufaransa, Louis Nicollin amesema anatarajia kuzungumza na nguli wa soka wa Argentina Diego Maradona kuhusu suala la kukinoa kikosi hicho msimu ujao. Klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo ambayo imeshinda taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia yake msimu uliopita, inatafuta kocha atakayeziba pengo wa kocha wa sasa Rene Girard ambaye mkataba wake unaishia mwishoni mwa msimu huu. Nicollin amesema Maradona amekuwa akifikiria kufundisha soka Ulaya na labda katika klabu hiyo na kama atataka kuzungumza nao watampokea kwa mikono miwili. Bosi huyo wa Montpellier amekiri kukumbwa na changamoto nyingi baada ya mawakala wengi kujitokeza kudai kuwa wanafanya kazi kwa niaba ya Maradona lakini anaamini suala hilo linaweza kupata suluhu pale nyota huyo atapokwenda na wakala kufanya mazungumzo. Maradona kwasasa anaishi jijini Dubai ambako anafanya kazi kama balozi katika baraza la michezo la mji huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment