Friday, March 8, 2013

GOLIKIPA WA ZAMANI FLAMENGO AHUKUMIWA MIAKA 22 JELA KWA MAUAJI.

MCHEZA soka nyota wa Brazil, Bruno Fernandes amehukumiwa miaka 22 jela kwa kukutwa na kosa la kuamuru mauaji ya rafiki yake wa kike wa zamani. Nyota huyo pia alikutwa na hatia ya kuuficha mwili wa Eliza Samudio na kumteka mtoto wao wa kiume mwaka 2010. Fernandes ambaye ni golikipa wa zamani wa klabu ya Flamengo alikiri kufahamu kuwa Samudio alinyongwa na mwili wake kupewa mbwa wale lakini alikataa kutoa amri ya kumuua mwanamke huyo. Mauaji hayo yalivutia vyombo vingi vya habari vya Brazil ambapo yalikuwa yakifananishwa na kesi ya OJ Simpson huko Marekani. Fernandes ambaye alikuwa maarufu kwa mashabiki wa soka wan chi hiyo alikuwa akipigiwa chepuo kucheza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014. Mmoja wa marafiki zake, Luiz Henrique Ferreira Ramao na polisi wa zamani Marcos Aparecido dos Santos nao pia walihukumiwa kutokana na mauaji ya Samudio.

No comments:

Post a Comment