Friday, March 8, 2013
TEVEZ MATATANI KWA KUENDESHA.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa kutoka Argentina, Carlos Tevez ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuendesha gari wakati hastahili na kama akishitakiwa na kukutwa na hatia ya kufanya tukio hilo anaweza kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Uingereza Tevez mwenye umri wa miaka 29 ambaye alifungiwa kuendesha gari Januari mwaka huu alisimamishwa na polisi katika mitaa ya Macclesfield karibu na jiji la Manchester jana. Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizosambaa nyota huyo ambaye anacheza katika klabu ya Manchester City amechiwa kwa dhamana lakini hakuna mhusika yoyote kutoka ndani ya klabu aliyepatikana kuzungumzia suala hilo. Tevez alikuwa na hatia ya makosa mawili ya kushindwa kupeleka taarifa zilizohitajika baada ya gari lake kukamatwa likiwa katika mwendo kasi ambapo mbali na kufungiwa miezi sita lakini pia alitozwa faini ya paundi 1,540. Mawakili waliokuwa wakimtetea nyota huyo walimwambia hakimu wa mahakama ya Manchester kuwa mteja wao hakuelewa baadhi ya maneno ambayo yalikuwa yameandikwa katika barua aliyotumiwa na polisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment