Friday, March 8, 2013

JORDAAN KUOGOMBEA TENA NAFASI CAF.

ALIYEKUWA msimamizi wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Afrika mwaka 2010, Danny Jordaan ameingia katika kinyang’anyiro cha kutafuta nafasi ya ujumbe katika kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF. Jordaan atagombea nafasi hiyo katika kikao cha kamati kuu ya shirikisho hilo kitakachofanyika jijini Marrakech, Morocco Jumapili ambapo amejinadi kubwa ana nafasi kubwa ya kutwaa nafasi hiyo. Hii ni mara ya pili kwa Jordaan kugombea nafasi hiyo nyeti katika soka la Afrika baada ya kugaragazwa miaka miwili iliyopita katika uchaguzi uliofanyika nchini Sudan. Pia alishindwa katika nafasi ya mmoja wa wawakilishi wa Afrika katika kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA baada ya kujitoa dakika za mwisho baada kukumbwa na kashfa. Lakini safari hii Jordaan mwenye umri wa miaka 61 ana nafasi kubwa ya kushinda baada ya uamuzi wa kuongeza nafasi katika kamati kwa mwakilishi kutoka nchi zilizo kusini mwa Afrika. Uchaguzi huo ndio ajenda pekee katika mkutano mkuu huo na utashuhudia rais wa CAF Issa Hayatou kuchaguliwa tena bila kupingwa kwa kipindi cha minne mingine. Juhudi za mpinzani wake Jacques Anouma kujaribu kupindua uamuzi wa kuwatoa wajumbe wasio katika kamati ya utendaji kwenye uchaguzi zilishindikana mapema wiki hii baada ya kukataliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS.

No comments:

Post a Comment