Friday, March 8, 2013

XAVI AANZA MAZOEZI.

KLABU ya Barcelona imepata ahueni kabla ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan utakaofanyika Jumanne ijayo baada ya kiungo wake Xavi Hernandez kurejea mazoezini kufuatia majeraha ya misuli yaliyokuwa yakimsumbua. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye alikosa mchezo wa La Liga dhidi ya Real Madrid mwishoni mwa wiki iliyopita, alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza maema Ijumaa. Kocha msaidizi wa Barcelona, Jordi Roura ambaye anashikilia nafasi ya Tito Vilanova ambaye yuko katika matibabu ya kansa huko jijini New York amesema wanatarajia kutoa uamuzi mwishoni kama kiungo huyo atajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo ambacho kitakwaana na Deportivo La Coruna Jumamosi. Barcelona inahitaji kupambana katika mchezo wa marudiano dhidi ya AC Milan baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza kama wanahitaji kuweka matumaini yao hai ya kunyakuwa taji la tano la michuano hiyo ya Ulaya.

No comments:

Post a Comment