Tuesday, March 26, 2013

VILANOVA ATUA BARCELONA.

KLABU ya Barcelona ya Hispania, imetangaza kuwa kocha wa klabu hiyo ambaye alikuwa jijini New York kwa matibabu ya kansa toka Januari mwaka huu amerejea nchini humo leo. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imethibitisha kuwa kocha huyo tayari yuko jijini Barcelona tayari kuendelea kuendelea na majukumu yake katika klabu hiyo baada ya kuwa nje kwa kipindi cha miezi miwili. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 aliondoka kwenda New York kwa matibabu zaidi ya mionzi Januari na katika kipindi hichochote msaidizi wake Jordi Roura ndio alikuwa akiisimamia timu hiyo. Taarifa hiyo pia ilidai kuwa Roura na Aureli Altimira ambao ndio waliompokea Vilanova wakati aliporejea ndio wataongoza mazoezi ya timu hiyo leo mchana huku Vilanova mwenyewe akitarajiwa kuchukua nafasi yake hatua kwa hatua.

No comments:

Post a Comment