Tuesday, March 26, 2013

10,000 KURUHUSIWA KUISHANGILIA MISRI.

MASHABIKI wapatao 10,000 wanatarajiwa kuruhusiwa kuishangilia timu yao ya taifa ya Misri wakati wa mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Zimbabwe ikiwa ni hatua moja kubwa ya kuirejesha nchi hiyo katika hali ya kawaida kimichezo. Misri pia wanafikiri uwepo wa mashabiki uwanjani katika mchezo huo utaongeza nafasi yao ya kufuzu michuano hiyo itakayofanyika nchini Brazil mwkaani kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya 20 kupita. Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo inatarajia kuruhusu idadi hiyo ya mashabiki katika Uwanja wa Borg El Arab uliopo katika pwani ya Mediterranean toka walipozuia kufanya hivyo baada ya vurugu za kisiasa zilizopelekea mashabiki wapatao 70 kupoteza maisha katika mchezo wa ligi huko Port Said mwaka mmoja uliopita. Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Misri toka kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa rais wan chi hiyo kwa kipindi kirefu Hosni Mubarak pia viliathiri soka na kupeleka kushindwa kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kipindi cha miaka miwili.

No comments:

Post a Comment