Tuesday, March 26, 2013

BRAZIL BADO IKO VIZURI - SCOLARI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amesisitiza kuwa kikosi chake kiko katika njia sahihi baada ya kutoa sare dhidi ya Urusi Jumatatu usiku. Brazil ilihitaji bao la dakika za mwisho lilifungwa na mshambuliaji wa klabu ya Fluminense Fred ili kupata sare hiyo kutoka kwa Urusi inayonolewa na kocha Fabio Capello katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika katika Uwanja wa Stamford Brigde. Scolari ameshindwa kuipa ushindi Brazil toka achukue mikoba tena ya kuinoa ambapo mbali na sare hiyo lakini pia alitoa sare ya mabao 2-2 na Italia wiki iliyopita huku akikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Uingereza Februari mwaka huu. Akihojiwa mara ya mchezo huo Scolari amesema kuwa katika mechi dhidi ya Italia na Urusi wamecheza kwa kiwango kizuri lakini aliwataka watu wasisahau kuwa walikuwa wakicheza na timu ambazo zilikuwa zimejipanga vizuri. Brazil inakabiliwa na mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Chile April 24.

No comments:

Post a Comment