Tuesday, March 26, 2013

KOCHA WA DRC ALALAMIKIA UMRI MKUBWA WA WACHEZAJI KATIKA MICHUANO YA VIJANA YA AFRIKA.

KOCHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC Sebastian Migan amebainisha kuwa timu yake ingesonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Vijana ya Afrika kama timu zingine zingefuata sheria. DRC ilishindwa kufuzu hatua hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Nigeria katika mchezo uliochezwa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Ahmed Zabana. Migan amedai kuwa baadhi ya timu katika michuano hiyo wamekuwa wakidanganya umri wa wachezaji wao na kutaka maofisa wanaosimamia michuano hiyo kulifuatilia kwa makini suala hilo. Kocha amesema iko wazi kwangu na kwa wengine kuwa wachezaji wengi katika timu ya Nigeria walikuwa wamezidi umri zaidi ya miaka 20 lakini amefurahishwa na jinsi wachezaji wake walivyojituma pamoja na kwamba wametolewa. Nigeria ambao wanatuhumiwa kutumia vijeba katika michuano hiyo wanatarajiwa kuchuana na Misri katika Uwanja wa Oumr Ouciaf baadae leo.

No comments:

Post a Comment