Tuesday, March 26, 2013

SHARAPOVA, SERENA HAWASHIKIKI MICHUANO YA SONY OPEN.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Urusi, Maria Sharapova amefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya wazi ya Sony kwa kumfunga Klara Zakopalova wa Jamhuri ya Czech. Sharapova alimfunga Zakopalova kwa 6-2 6-2 na kujikatia tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo inayofanyika huko Miami, Florida nchini Marekani. Mapema mwanadada anayeshika namba moja katika orodha za ubora wa mchezo huo Serena Williams naye alifanikiwa kusonga mbele baada ya kumfunga Dominika Cibulkova wa Slovakia. Katika mchezo huo Williams ilibdi atumie uzoefu wake baada ya kupoteza seti ya kwanza lakini alifanikiwa kuzinduka na kumfunga Cibulkova kwa 2-6 6-4 6-2.

No comments:

Post a Comment