Tuesday, March 26, 2013

WOODS KINARA WA GOFU DUNIANI KWA MARA NYINGINE.

MCHEZAJI gofu nyota Tiger Woods amerejea katika nafasi ya kwanza katika orodha za wachezaji bora wa mchezo huo duniani toka mwaka Octoba mwaka 2010 baada ya kushinda michuano ya Arnold Palmer Invitational. Woods mwenye umri wa miaka 37 alichukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Rory McIlrol aliyekuwa akishika nafasi hiyo toka Novemba mwaka 2011. Hilo linakuwa ni taji la 77 la mashindano ya PGA kwa Woods ambaye ni raia wa Marekani na tatu kwa mwaka huu 2013. Akihojiwa mara baada ya kushinda mchezo huo Woods amesema ilikuwa michuano mizuri na anafurahi kurejea katika nafsi ya kwanza baada ya kusota kurejea katika kiwango chake kwa kipindi kirefu. Amesema ushindi huo wa taji la PGA unamuweka vyema kabla ya kuanza kwa msimu mpya akijaribu kufukuzia taji la tano la michuano mikubwa ya Masters ambayo inatarajiwa kuanza April 11 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment