Tuesday, March 26, 2013

ENYEAMA ASHINDWA KUTIMIZA AHADI.

GOLIKIPA wa Nigeria, Vincent Enyeama amethibitisha kuwa alivunja ahadi yake ya kucheza huku akiwa amevua bukta yake kufuatia timu ya taifa ya nchi hiyo kunyakuwa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon iliyofanyika nchini Afrika Kusini. Katika mahojiano yake na mtandao wa supersport jijini Faro, Ureno mapema Januari, Enyeama alidai kuwa kama Nigerian ikitawazwa mabingwa wa Afrika ndoto zake zitakuwa zimetimia na kwa furaha atacheza huku akiwa amevua bukta yake. Lakini golikipa alipohojiwa kuhusu ahadi yake hiyo aliyotoa alidai kuwa hakuitmiza kwasababu haikumlazimu kufanya hivyo kwani sio ahadi zote zinezotolewa na serikali huwa zinatimizwa na hilo linakwenda sambamba na ahadi mbalimbali zinatolewa na watu. Enyeama ambaye ameichezea Nigeria mechi 78 za kimataifa amesema ana sababu zake binafsi za kushindwa kutimiaza ahadi yake aliyotoa mwenyewe.

No comments:

Post a Comment