Monday, March 4, 2013
VILANOVA KUMALIZA MATIBABU YAKE MIWSHONI MWA MACHI.
RAIS wa klabu ya Barcelona Sandro Rosell amesema kocha wa timu hiyo Tito Vilanova anatarajia kumaliza matibabu yake ya kansa jijini New York, Marekani na kurejea katika kibarua chake mwishoni mwa mwezi huu. Vilanova mwenye umri wa miaka 44, alihitaji kufanyiwa upasuaji wa pili Desemba mwaka jana baada ya upasuaji wa kwanza wa kuondoa uvimbe wa kansa katika tezi Novemba mwaka 2011 kutofanikiwa na msaidizi wake Jordi Roura ndio amechukua mikoba hiyo mpaka atakapopata nafuu. Ingawa Barcelona bado wanaongoza Ligi Kuu nchini Hispania kwa tofauti ya alama 11 lakini wamekuwa wakisuasua katika michezo yake ya hivi karibuni baada ya kufungwa mara mbili na mahasimu wao Real Madrid na pia kufungwa mabao 2-0 na AC Milan katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Rosell amesema Vilanova yuko katikati ya matibabu yake ya mionzi na wakati alipokwenda kumtembelea New York wiki iliyopita alimkuta katika hali nzuri na alikuwa akijihusisha na shughuli za kila siku za klabu hiyo pamoja na umbali aliopo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment