Monday, March 4, 2013
SUDAN YAGONGA MWAMBA CAS.
NCHI ya Sudan imeshindwa rufani yake dhidi ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ya kudai ushindi wao wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Zambia katika mchezo wa kufuzu michuano Kombe la Dunia Juni mwaka jana na wapinzani wao hao kuzawadiwa ushindi wa mabao 3-0. Uamuzi huo uliotangazwa na Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS jana unamaanisha kuwa Zambia itaongozwa kundi D katika mzunguko wa pili wa kufuzu kwa nchi za Afrika na kuwaacha Ghana wakisuasua kutafuta tiketi ya kushiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Brazil mwakani. FIFA iliikuta Sudan na makosa ya kumchezesha Saif Ali ambaye alifunga bao la pili la nchi hiyo pamoja na kuwa amefungiwa kucheza mechi za ushindani ambapo CAS walitupilia rufani ya Sudan ambao walidai kuwa hawakufahamishwa sawasawa juu ya kusimamishwa kwake. Mchezaji huyo alitolewa nje katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika iliyofanyika mwaka jana katika mchezo dhidi ya haohao Zambia na alikuwa hajamaliza kutumikia adhabu yake ya kutocheza mechi mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment