Monday, March 25, 2013

VILANOVA KUREJEA NYUMBANI BAADA YA MIEZI MIWILI YA MATIBABU.

KLABU ya Barcelona imebainisha kuwa kocha wake Tito Vilanova atarejea nyumbani wiki hii baada ya kukaa jijini New York Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu ya mionzi ya kansa. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alifanyiwa upasuaji wa koo kuondoa uvimbe wa kansa Desemba 20 mwaka jana na baadae kuanza tiba ya mionzi kwa muda wa wiki sita. Kocha aliondoka kuelekea New York kwa matibabu zaidi Januari na sasa yuko tayari kurejea nyumbani tena baada ya kukaa huko marekani kwa miezi miwili. Vilanova alichukua nafasi ya Pep Guardiola katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka jana na kupewa mkataba wa mwaka mmoja ambapo wakati akiwa katika matibabu nafasi yake ilikuwa ikishikiliwa na kocha msaidizi Jordi Roura.

No comments:

Post a Comment