Monday, March 25, 2013

FRANKFURT YAMUONGEZA MKATABA VEH.

KLABU ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani imebainisha kuwa kocha Armin Veh amekubali kuongeza mkataba wa kuinoa klabu hyo kwa msimu mwingine mmoja mpaka mwaka 2014. Veh ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka 2011 aliiongoza timu hiyo kurejea katika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Bundesliga ambapo sasa timu hiyo inafukuzia nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika taarifa iliyotolewa na rais wa klabu hiyo Heribert Brunchhagen amesema amefurahi kumshawishi kocha huyo kuendelea kuwepo hapo haswa kutokana na kuingoza vyema klabu hiyo msimu huu. Mbio za Frankfurt msimu huu ni kutafuta nafasi ya nne lakini Veh amepania kukisuka upya kikosi chake msimu ujao kwa ajili kutafuta nafasi za juu zaidi au kunyakuwa taji la Bundesliga.

No comments:

Post a Comment