Monday, March 25, 2013

MUNTARU AWAPONGEZA MASHABIKI JIJINI KUMASI.

NAHODHA wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana, Sulley Muntari amewapongeza mashabiki wa soka wa nchi hiyo waliojitokeza kuishangilia timu yao wakati wakicheza mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe ya Dunia dhidi ya Sudan uliofanyika katika Uwanja wa Baba Yara jijini Kumasi. Katika mchezo huo Ghana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 na kuweka matumaini hai ya kukata tiketi ya kucheza michuano hiyo ambapo Muntari alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza toka aumie mguu. Muntari amesema ushindi huo ulikuwa mzuri kwao kwasababu Zambia ambao wako nao kundi moja wenyewe walitoka bila ya kufungana na Lesotho, na ushindi huo utawasaidia katika mchezo mwingine wa ugenini dhidi ya hao hao Sudan na ni mategemeo yao watashinda tena. Mabao ya Ghana katika mchezo huo yalifungwa na Asamoah Gyan, Mubarak Wakaso, Abdul Majeed Waris na Emmanuel Badu na ushindi huo unaifanya Ghana kuisogelea Zambia ambao wanaongoza kundi lao kwa tofauti ya alama moja huku kukiwa kumebakia michezo mitatu.

No comments:

Post a Comment