Monday, March 25, 2013

WACHEZAJI WA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI WASHINDWA KUREJEA NYUMBANI BAADA YA WAASI KUCHUKUA NCHI.

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wanatarajiwa kuchelewa kurejea nyumbani baada ya waasi kuuteka mji mkuu wa nchi hiyo wakati wachezaji hao wakiwa Afrika Kusini kucheza mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia. Chama cha Soka nchini Afrika Kusini-SAFA kimesema kuwa timu hiyo inatarajiwa kuondoka nchini humo kwa makundi mawili lakini hakuna kundi hata moja litakaloelekea nyumbani kwasasa. Wachezaji wan chi hiyo wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya watasafiri kuelekea Paris baadae leo, wakati wachezaji wanaosakata kabumbu nyumbani wao watakwenda Douala, Cameroon ambapo watakuwa wakifuatilia hali inavyoendelea nyumbani. Majeshi ya waasi yalifanikiwa kuuteka mji mkuu wan chi hiyo Bangui na kumlazimisha rais aliyekuwepo madarakani kuikimbia nchi yake. Afrika ya Kati ilifungwa mabao 2-0 na Afrika Kusini katika mchezo huo uliochezwa jijini Cape Town Jumamosi.

No comments:

Post a Comment