Monday, March 25, 2013

PELE AFURAHISHWA NA JEMBE LAKE JOSHUA KUANZA KUNG'AA SANTOS.

NGULI wa soka duniani Pele ameonyesha furaha yake baada ya kumshuhudia mwanae wa kiume aitwaye Joshua akicheza katika kikosi cha klabu ya Santos kwenye michuano ya vijana chini ya miaka 17. Ili kuonyesha furaha yake Pele alitumwa picha ya mwanaye huyo mwenye umri wa miaka 16 katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter na kusema kuwa amefurahishwa kumuona mwanae akiwa katika jezi ya Santos. Katika kipindi chake Pele alifunga mabao zaidi 1,000 wakati akicheza Santos na anajulikana kama mmoja wa wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika kipindi chote. Pele alisajiliwa Santos akiwa na umri wa miaka 15 na kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kushinda Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 17. Wakati akifunga bao lake ya 1000 Novemba 19 mwaka 1969 mashabiki wa Santos walivamia uwanja na kumbeba juu juu na siku imebakia katika kumbukumbu za klabu hiyo ambayo huitwa Pele Day.

No comments:

Post a Comment