Monday, March 25, 2013

VETTEL AMUOMBA RADHI WEBBER.

DEREVA wa mbio za magari ya langalanga, Sebastian Vettel amemuomba radhi dereva mwenzake wa timu ya Red Bull Mark Webber kwa kumpita na kwenda kinyume na maagizo aliyopewa na kupelekea kushinda mbio za Malaysian Grand Prix. Katika mbio hizo Vettel alipewa maagizo na timu yake kupunguza mwendo kwasababu Webber tayari alikuwa akiongoza mbio hizo katika mzunguko wa mwisho lakini dereva huyo alikaidi maagizo hayo kwa kuongeza kasi na kumpita mwenzake na kunyakuwa ubingwa wa mbio hizo. Vettel amesema anajua hakufanya vyema kukaidi amri aliyopewa, haelewi ni kwanini alimua kufanya hivyo ila anaomba radhi kwa timu nzima pamoja na dereva mwenzake. Dereva huyo aliendelea kusema kuwa anajua anahitaji kuwa na maelezo ya kutosha juu ya kilichotokea kwasababu alisikia maelezo aliyopewa vizuri lakini hakuyatekeleza kwasasabu hakuelewa ndio kitu pekee ambacho anaweza kusema kwasasa. Mbio hizo ambazo zilifanyika katika mvua iliyokuwa ikinyesha katika jiji la Kuala Lumpur Vettel alishika namba moja akifuatia wa Webber na nafasi ya tatu ilishikwa na Lewis Hamilton wa timu ya Marcedes.

No comments:

Post a Comment