AC MILAN HAITAUZWA NG'O - BARBARA BERLUSCONI.
 |
BARBARA BERLUSCONI. |
FAMILIA ya rais wa klabu ya AC Milan ya Italia, Silvio Berlusconi imedai kuwa haina mpango wa kuiuza klabu hiyo kwa mtu yoyote Yule. Mkurugenzi wa klabu hiyo ambaye pia ni binti wa Berlusconi aitwaye Barbara amesema baba yao aliwafundisha kila kitu kuwa klabu hiyo ina nafasi katika mioyo yao hivyo hawawezi kuiuza klabu hiyo. Barbara amesema kutengeneza ushirika kwa ajili ya uwekezaji ili kuikuza klabu hiyo inewezekana lakini kuuza klabu moja kwa moja hili halitawezekana kamwe. Kulikuwa na tetesi mwaka uliopita kuwa Milan inafikiria kuuza baadhi ya hisa zake kwa kampuni moja nchini Qatar lakini makamu wa rais wa klabu hiyo Adriano Galliani alikatana tetesi hizo na kudai kuwa sio za kweli. Milan imekuwa na msimu wa kutia moyo baada ya kuanza vibaya mwanzoni lakini hivi sasa wako katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A huku wakicheza michezo 12 bila kufungwa.
No comments:
Post a Comment