MSHABIKI wa soka wa klabu ya Arsenal, amefungiwa kuhudhuria mechi za soka kwa muda wa miaka mitatu baada ya kukiri kurusha ganda la ndizi kwenda shambuliaji wa Tottenham Hotspurs Gareth Bale katika mchezo wa timu hizo mahasimu kaskazini mwa London. Thomas Flint alishtakiwa na jaji kwa tabia ya kudhalilisha aliyoionyesha kwa kumrushia ganda la ndizi Bale ambaye ni mweupe wakati akipiga mpira wa kona kwenye mechi ya ligi iliyofanyika katika Uwanja wa White Hart Lane, Machi 3 mwaka huu. Mbali na adhabu hiyo Flint pia alitozwa faini ya paundi 250. Arsenal mara kwa mara imekuwa ikisema kuwa itamfungia maisha kushuhudia mechi zake mshabiki yoyote atakayekutwa na hatia ya kufanya vitendo vya kibaguzi.
No comments:
Post a Comment