Friday, April 12, 2013

RICHARDS NAYE AINGIA KUNDI LA KINA TEVEZ NA NASRI.

ORODHA ya wachezaji wa klabu tajiri ya Manchester City kufungiwa kuendesha magari kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani imeongezeka baada ya Micah Richards naye kufungiwa kuendesha gari miezi sita. Carlos Tevez na Samir Nasri tayari wamepewa adhabu inayofanana na hiyo wiki iliyopita, huku Tevez pia akiamriwa kufanya kazi za kijamii kwa saa 250 kwa kuendesha wakati amefungiwa na bila leseni. Richards alikiri makosa mawili ya kushindwa kumtaja aliyekuwa akiendesha gari lake aina ya Ferrari ambalo lilikamatwa likiwa katika mwendo mkali jijini Manchester, Septemba mwaka jana. Mchezaji alijitetea kuwa alishindwa kuepeleka vielelezo vilivyohitajika kwa muda kutokana na shughuli nyingi zilizomtinga.

No comments:

Post a Comment