Tuesday, April 16, 2013

BARCELONA WANATUHOFIA - HOENESS.

RAIS wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, Uli Hoeness amekiri kuwa timu yake hiyo inakabiliwa na kibarua kigumu cha kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuitoa Barcelona lakini anaamini kuwa hata wapinzani wao hawajafurahishwa kupangwa nao. Hoeness ambaye alikuwa mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa West Germain amekiri kuwa Barcelona ni timu ambayo kikosi chake ilikuwa haitaki kukutana nayo lakini akadai kuwa kama wanahitaji kunyakuwa taji la Ulaya lazima wamfunge mpinzani yoyote wanaekutana naye. Hoeness amesema kupangwa na Barcelona ni jambo gumu na walitegemea wangeanzia ugenini katika mchezo wao wa kwanza lakini na hilo halikutokea hivyo kufanya mambo kuwa magumu zaidi. Amesema pamoja na ugumu huo lakini hawana jinsi kama wanahitaji taji lazima wamfunge yoyote wanayekutana naye na ana uhakika kuwa Barcelona pia wanawahofia kupambana nao kama ilivyo kwao. Mechi ya kwanza baina ya timu hizo mbili inatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Allianz Arena April 23 kabla ya kurudiana tena wiki moja baadae katika Uwanja wa Camp Nou.

No comments:

Post a Comment