Tuesday, April 16, 2013

PAMOJA NA MILIPUKO YA BOSTON MARATHON, MASHINANO YA LONDON MARATHON KUENDELEA KAMA KAWAIDA.

MASHINDANO ya London Marathon yanatarajia kufanyika kama kawaida siku ya Jumapili pamoja na tukio la kutisha la kulipuka kwa mabomu lilitokea katika mbio za Boston Marathon na kuacha watu watatu wakipoteza maisha na mamia wengine wakijeruhiwa. Tukio hilo la kuogofya limetokea zikiwa zimebakia siku sita kabla ya wanariadha zaidi ya 10,000 hawajakusanyika katika mitaa ya London kwa ajili ya mashindano hayo. Waziri wa Michezo nchini Uingereza, Hugh Robertson amesisitiza kuwa wanajiamini kwa asilimia mia moja kwamba michuano ya London Marathon itakuwa salama. Robertson amesema wamejiandaa kikamilifu na wameongeza ulinzi maradufu katika mitaa mbalimbali ambayo wanariadha watakuwa wakipita ili kuhakikisha usalama na ni mategemeo yao mbio hizo zitamalizika salama. Katika mlipuko wa mabomu uliotokea katika mbio za Boston Marathon nchini Marekani watu watatu walifariki na wengine zaidi ya 140 kujeruhiwa huku 17 kati yao wakiwa katika hali mbaya baada ya kukatika sehemu mbalimbali za viungo vyao.

No comments:

Post a Comment