
Tuesday, April 16, 2013
NILIHARAKISHA KUMCHEZESHA WILSHERE - WENGER.
KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa aliharakisha kumrejesha Jack Wilshere aliyekuwa ameumia kwa kumchezesha katika mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Norwich City. Wilshere mwenye umri wa miaka 21 aliingia dimbani kwa mara kwanza toka aumie kifundi cha mguu katika mchezo baina ya timu hiyo dhidi ya mahasimu wao Tottenham Hotspurs uliochezwa Machi 3 mwaka huu. Wenger ambaye kikosi chake kinakabiliwa na kibarua kigumu baadae leo katika mchezo wa ligi dhidi ya Everton, amesema aliharakisha kumrejesha nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza kwani bado hakuwa tayari. Kocha huyo ambaye timu yake ina ukame wa vikombe kwa kipindi cha miaka nane aliendelea kusema kuwa ataomba ushauri katika kitengo cha tiba na kumuuliza mwenyewe anavyojisikia halafu atatumia zoefu wake. Wilshere amecheza mechi 27 kwa timu yake msimu huu baada ya kukosa msimu mzima wa mwaka 2011-2012 kutokana na tatizo la kifundo cha mguu wake mwingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment