MWANARIADHA nyota wa mbio fupi, Usain Bolt ameipongeza klabu ya Bayern Munich kwa kuweka rekodi rekodi ya kunyakuwa taji la Bundesliga mapema zaidi na kuipa nafasi ya kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Bolt amesema Bayern imekuwa katika kiwango bora msimu huu na kudai kuwa ni kitu cha kipekee kushinda taji la ligi ngumu kama hiyo kwa pengo kubwa la alama halafu mapema. Bolt ambaye ashikilia rekodi ya dunia katika michuano ya Olimpiki yam bio za mita 100, 200 na za mita 400 kupokezana vijiti mara kwa amara anakwenda jijini Munich kwa ajili ya matibabu kutoka daktari wa Bayern Hans-Wilhelm Mueller-Wohlfahrt. Nyota huyo ambaye ni shabiki mkubwa wa soka pia alikutana na baadhi ya wachezaji kama Bastian Schweinsteiger. Pia amesema anaamini kuwa Bayern wana nafasi kubwa ya kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kama wataendelea kucheza katika kiwango cha juu kama hivi sasa ingawa timu za Real Madrid na Barcelona zinaonekana nazo ziko vizuri.
No comments:
Post a Comment