Sunday, April 7, 2013

BONDIA AFARIKI BAADA YA KIPIGO.

BARAZA la Udhibiti wa Mchezo wa Ngumi nchini Uingereza, BBBC limethibitisha kutokea kifo cha bondia Michael Norgrove siku chache baada kuanguka akiwa ulingoni. Bondia huyo wa uzito mwepesi raia wa Zambia ambaye ameweka makazi yake jijini London alianguka ulingoni Machi 31 mwaka huu. Norgrove alikuwa akitibiwa kudhibiti damu iliyovilia katika ubongo kufuatia pambano lake na bondia Tom Bowen lililofanyika katika mji wa Blackfriars uliopo kusini mwa London. Katibu Mkuu wa BBBC Robert Smith alithibitisha kutokea kwa kifo cha bondia huyo na kukielezea kama siku ya majonzi zaidi katika mchezo wa masumbwi duniani.

No comments:

Post a Comment