
Wednesday, April 17, 2013
BOLT KUSHIRIKI DIAMOND LEAGUE LONDON.
MWANARIADHA nyota wa mbio fupi, Usain Bolt anatarajiwa kurejea tena jijini London kushindana katika mbio za IAAF Diamong League zitakazofanyika katika Uwanja wa Olimpiki ambao alifanikiwa kunyakuwa medali za dhahabu mwaka uliopita. Bolt ambaye ni bingwa mara sita wa michuano ya olimpiki ataongoza mbio zikiwa ni sherehe za kutimiza mwaka mmoja toka kufunguliwa michuano ya olimpiki mwaka jana. Mbio zitafanyika kuanzia Julai 26 hadi 28 na zitashirikisha wanariadha 29 waliopata medali katika michuano ya olimpiki, wakiwemo wanariadha 12 walionyakuwa medali za dhahabu na wengine wanne waliovunja rekodi za dunia katika michuano hiyo. Kwenye mashindano hayo Bolt ambaye atashiriki katika mbio za mita 100 na mita 400 kupokezana vijiti atayatumia mashindano hayo kama maandalizi kwa ajili ya mshindano ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow Agosti mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment