Friday, April 19, 2013

CARRICK NDANI KATIKA ORODHA YA WACHEZAJI BORA WA MWAKA UINGEREZA.

KIUNGO nyota wa Manchester United Michael Carrick ametajwa katika orodha ya wachezaji wa kulipwa wanagombania tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka. Mbali na Carrick wengine waliomo katika orodha hiyo ni pamoja na Gareth Bale wa Tottenham Hotspurs, Robin van Persie wa United, Luis Suarez wa Liverpool, Eden Hazard na Juan Malta wote wa Chelsea. Kwa upande wa wanaogombania tuzo hiyo kwa wachezaji chipukizi ni pamoja na Christian Benteke wa Aston Villa, Romelu Lukaku wa West Bromwich, Danny Welberg wa United na Jack Wilshere wa Arsenal huku Bale na Hazard nao pia wakiwemo katika tuzo hizi za wachezaji chipukizi. Bale alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wakubwa mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 21 wakati Van Persie yeye alishinda tuzo hiyo mwaka jana akiwa Arsenal.

No comments:

Post a Comment