
Friday, April 19, 2013
MCLAREN WALINITIMUA KATIKA KARAKANA YAO - HAMILTON.
DEREVA nyota wa magari yaendayo kasi ya langalanga, Lewis Hamilton amedai kuwa aliamriwa kutoka nje ya karakana ya magari ya McLaren wakati alipokuwa akitaka kuwatembelea wafanyakazi wenzake wa zamani katika majaribio ya kipindi cha baridi. Hamilton ambaye ni raia wa Uingereza alisitisha mkataba wake na MacLaren ambao alifanya nao kazi kwa kipindi cha miaka 14 baada ya kusaini mkataba mpya na timu ya Marcedes. Uhamisho huo wa Hamilton ambao ulileta utata unaonekana kumuendea vyema kutokana na Marcedes kuonekana kuizidi McLaren katika hatua za mwanzoni mwa msimu huu. Hamilton amesema alienda kuwaona wakati wakiwa Australia na pia alijaribu tena kwenda wakati wakiwa Hispania lakini Mkurugenzi wa Michezo wa MacLaren, Sam Michael alimfukuza kwa kumtaka kutoka nje ya karakana yao. Hamilton kitendo hicho alichofanyiwa na Michael hakikumfurahisha hata kidogo na amejisikia vibaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment