RAIS wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell amebainisha kuwa amepanga kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kingine pindi atakapomaliza kipindi cha kwanza mwaka 2016. Rosell alichaguliwa kuwa rais wa klabu hiyo ya Hispania mwaka 2010 ambapo hapo kabla alikuwa mjumbe wa bodi katika uongozi wa aliyekuwa rais wa klabu hiyo Joan Laporta kabla ya kujiuzulu mwaka 2005. Chini ya uongozi wa Rosell Barcelona imefanikiwa kushinda taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, taji lingine moja la Ligi Kuu nchini Hispania na moja la Kombe la Mfalme ambapo msimu huu wako katika nafasi ya kunyakuwa taji lingine la ligi huku wakiwa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barcelona inamilikiwa na maelfu ya wanachama ambao huchagua rais na kamati ya utendaji, uchaguzi ambao hufuatiliwa kwa karibu na mashabiki wa soka wa mji huo na nchi nzima kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment