Friday, April 19, 2013

MASHABIKI WA SOKA ARGENTINA WAWAVAMIA WACHEZAJI BAADA YA TIMU YAO KUFUNGWA.

MASHABIKI kadhaa wa soka wa klabu ya Huracan ya Argentina wamevamia vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji baada ya mazoezi na kuwashambulia baadhi ya wachezaji. Mashabiki hao pia waliiba baadhi ya vitu vya wachezaji hao na kuharibu magari yao yaliyokuwa yameegeshwa nje ya uwanja uliopo katika mji mkuu wan chi hiyo Buenos Aires. Hatua ya mashabiki hao imefikiwa kutokana na matokeo mabaya ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata katika siku za karibuni. Huracan ambayo inashiriki ligi draja la pili nchini humo ilitolewa katika Kombe la Argentina na klabu ya ligi daraja la kwanza ya Godoy Cruz kwa changamoto ya mikwaju ya penati Jumatano iliyopita. Rais wa klabu hiyo Alejandro Nadur alilaani vikali vitendo vya kihalifu vilivyofanywa na mashabiki wao na kudai kuwa hata kama wangefungwa mabao 15 mashabiki hao hawakupaswa kufanya uhalifu huo.

No comments:

Post a Comment