Friday, April 19, 2013

MASHINDANO YA BAHRAIN GRAND PRIX USALAMA NI WA KUTOSHA - AL ZAYANI

MWENYEKITI na mratibu wa michuano ya magari yanayokwenda kasi ya langalanga ya Bahrain Grand Prix, Zayed Al Zayani amesema kuwa hakuna kitu chochote cha kuhofia kuhusiana na usalama wa timu pamoja na madereva kwenye mashindano hayo. Al Zayani amesema mara zote mashindano hayo yamekuwa yakifanyika katika hali ya kiusalama na mwaka huu hakutakuwa na tofauti yoyote. Mashindano ya Bahrain Grand Prix 2011 yalifitwa kutokana na machafuko yaliyopo huko lakini mwaka jana waliruhusiwa kuandaa tena baada ya kuhakikisha kwamba usalama ulikuwepo. Al Zayani amesema mashindano hayo ni muhimu kwani huinua uchumi wa Bahrain kutokana na fedha za kigeni wanazopata.

No comments:

Post a Comment