Friday, April 19, 2013

MONTE CARLO MASTERS: MURRAY CHALI.

MCHEZAJI nyota namba moja wa Uingereza, Andy Murray ameshindwa kusonga mbele katika hatua ya nane bora baada ya kukubali kipigo cha 6-1 6-2 kutoka kwa Stanislas Wawrinka katika mzunguko wa tatu wa michuano ya Monte Carlo Masters inayoendelea huko Monaco. Murray ambaye ameshinda mara nane katika mechi 12 walizokutana Wawrinka wa Switzerland katika mchezo huo alionekana kucheza chini ya kiwango chake cha kawaida nafasi ambayo ilitumiwa vyema na mpinzani wake kuhakikisha anaibuka kidedea. Kupoteza mchezo huo ni pigo kubwa kwa Murray ambaye alikuwa akitumia michuano hiyo kujiandaa kwa ajili ya kutetea taji lake la michuano ya wazi ya Ufaransa. Kwa upande mwingine Novak Djokovic na Rafael Nadal wao walifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kushinda mechi zao.

No comments:

Post a Comment