Thursday, April 11, 2013

FIFA YAITAKA GABON KURUDIA UCHAGUZI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetengua ushindi wa rais mpya wa Shirikisho la Soka nchini Gabon Jean de Dieu Moukagni baada ya mpinzani wake kukata rufani kupinga matokeo ya kura zilizopigwa. Pierre-Alain Mounguengui ambaye alipoteza uchaguzi huo kwa tofauti ya kura sita, alilalamika kukiukwa kwa utaratibu na udanganyifu kwenye uchaguzi huo. Mwakilishi wa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF na FIFA alisafiri kwenda jijini Libreville kutoa taarifa juu ya uamuzi huo mpya uliofikiwa na uchaguzi mwingine unatarajiwa kufanyika katika wiki chache zijazo. Moukagni alichaguliwa Machi 27 mwaka huu kwa kipindi cha miaka minne akichukua nafasi ya Placide Engandzas.

No comments:

Post a Comment