
Thursday, April 11, 2013
XAVI AVUNJA REKODI YA KUPIGA PASI NYINGI.
PAMOJA na Barcelona kushindwa kuonyesha kiwango chake bora katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya michuano Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint Germain lakini kiungo wa timu hiyo Xavi Hernandez alikuwa na usiku mzuri baada ya kufanikiwa kuweka rekodi ya kupiga pasi 96 katika mchezo huo. Barcelona ilibidi wapambane ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuwa nyuma kwa bao moja lakini walifanikiwa kusonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini baada ya Pedro kusawazisha katika dakika 71 na kufanya timu hizo kutoka sare kwa kufungana bao 1-1. Watu wengi waliotizama mchezo huo watasema kuingia kwa Lionel Messi katika kipindi cha pili ndio kulikoisaidia timu hiyo kufanya vizuri lakini alikuwa ni Xavi ambaye alicheza kwa kiwango cha juu kwenye nafasi ya kiungo kwa kupiga pasi nyingi na zenye uhakika. Juhudi za Xavi zilipelekea kuweka rekodi hiyo na kumpita Javier Zanetti aliyepiga pasi 72 katika mchezo kati ya Inter Milan na Tottenham Hotspurs uliochezwa miaka mitatu iliyopita pamoja na Emmanuel Eboue aliyepiga pasi 56 katika mchezo kati ya Porto na Arsenal mwaka 2006.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment