Thursday, April 11, 2013

SIKUOMBA RADHI KWA KUSHINDA MALAYSIA GRAND PRIX - VETTEL.

BINGWA wa dunia wa mashindano ya magari yanayokwenda kasi ya langalanga, Sebastian Vettel amesema kuwa hakuomba msamaha kwa kushinda mbio za Malaysia Grand Prix ambazo alikataa kutii amri ya timu yake ya Red Bull. Vettel aliambiwa na timu yake kusimama katika kituo wakati dereva mwenzake Mark Webber akiwa anaongoza lakini dereva huyo alikataa kutii amri hiyo na kumpita mwenzake na kushinda mbio hizo. Baadae Vettel aliomba radhi kwa kumpita mwenzake na ofisa mkuu wa Red Bull Helmut Marko kudai kuwa wameshasuluhisha tatizo hilo lakini wakati wakielekea katika mashindano ya China Grand Prix, Vettel ameibuka na kudai kuwa hakuomba radhi kwa kushinda. Vettel amesema aliomba radhi kwa kushindwa kutii amri aliyopewa na timu yake lakini sio kwa kushinda mbio hizo kwasababu ameajiriwa kwa kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment