Tuesday, April 30, 2013
HAVELANGE ATAJWA KULA MLUNGULA, BLATTER ASAFISHWA.
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Joao Havelange wa Brazil ambaye aliiongoza shirikisho hilo kwa zaidi ya miongo miwili, amejiuzulu wadhifa wake wa rais wa heshima aliopewa baada ya kutajwa kupokea mlungula. Taarifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na kamati ya maadili ya FIFA kuhusiana na sakata la wabia wao wa masoko-ISL ambapo Havelange ametajwa pamoja wajumbe wawili wa zamani wa kamati ya utendaji Ricardo Teixeira na Nicolas Leoz kupokea rushwa. Mwenyekiti wa tume hiyo maalumu uliyotolewa kusimamia sakata hilo Hans-Joachim Eckert pia alimtaja rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter kwamba alikuwa mzito kushughulikia suala hilo lakini akasema kwamba hajavunja sheria zozote za maadili ya shirikisho hilo. Pamoja na ripoti hiyo kusafisha Blatter ambaye kipindi wakati Havelange akiwa madarakani yeye alikuwa katibu mkuu wa FIFA wadau wengi wa soka bado wanaona rais huyo naye alihusika kwa namna moja au nyingine kutokana na nafasi aliyonayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment