Wednesday, April 3, 2013

KROOS NJE MSIMU MZIMA.

Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani inatarajia kukosa huduma ya kiungo wake wa kati Toni Kroos kwa msimu mzima uliobakia baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani kuumia kinena katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus. Kroos mwenye umri wa miaka 23 alipata maumivu hayo katika mguu wa kushoto katika dakika ya 13 ya mchezo huo ambao Bayern ilishinda kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Alianz Arena. Daktari wa Bayern, Hans-Wilhelm Mueller Wohlfahrt amesema kuwa Kroos atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita mpaka nane kutokana na ukubwa wa tatizo lililompata. Bayern ambayo inafukuzia kuwa timu ya kwanza nchini Ujerumani kushinda mataji yote matatu kwasasa wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa tofauti ya alama 20 na kuna uwezekano wa kunyakuwa Kombe la Ligi kama wataifunga Eintracht Frankfurt katika mchezo wa fainali Jumamosi.

No comments:

Post a Comment