
Wednesday, April 3, 2013
TEVEZ KUTUMIKIA JAMII KWA SIKU 250.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza, Carlos Tevez ameamriwa kufanya kazi za kijamii kwa saa 250 baada ya kukutwa na hatia ya kuendesha gari wakati amesimamishwa na bila bima. Tevez mwenye umri wa miaka 29 pia amefungiwa kuendesha gari kwa kipindi cha miezi sita na kutozwa faini ya paundi 1,000. Nyota huyo alikamatwa baada ya kukiuka adhabu yake ya kufungiwa kuendesha gari aliyopewa mara ya kwanza kwa kosa la kushindwa kujibu barua ya polisi kuhusu gari lake kukutwa katika mwendo kasi. Mahakimu hao walisikia kuwa tevez hakuwa na leseni ya udereva ya Uingereza kwasababu alikuwa akishindwa kufaulu majaribio aliyopewa ili kupata leseni ya kuendesha nchini humo. Tevez alikamatwa Machi 7 mwaka huu akiendesha gari bila bima na huku amefungiwa na kuelekwa katika kituo cha karibu ambapo baadae alitolewa kwa dhamana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment