
Wednesday, April 3, 2013
MESSI HATI HATI KUWEPO KUWAPOKEA PSG WIKI IJAYO.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi ameumia msuli wa paja wakati wa mchezo wa kwanza wa robo fainali kati ya timu yake na Paris Saint Germain ambao walikwenda sare kwakufungana mabao 2-2. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 25 ambaye aliifungiwa timu yake bao la kwanza katika dakika ya 38 aliumia dakika chache baadae na kulazimika kutolewa nje katika muda wa mapumziko. Messi ambaye alibadilishana na kiungo wa timu hiyo Cesc Fabregas anatarajiwa kufanyika vipimo zaidi ili kugundua ukubwa wa tatizo lake. Mbali na Messi Barcelona pia ilipata pigo lingine baada ya beki wake Javier Mascherano naye kutolewa nje kwa machela baada ya kuumia mguu wake wa kulia dakika ya 88 ya mchezo huo na anatarajiwa kukaa nje kwa kipindi cha wiki nne mpaka sita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment