
Tuesday, April 2, 2013
LIVERPOOL KUZURU THAILAND.
KLABU ya Liverpool kucheza mechi za kirafiki nchini Thailand ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na msimu wa 2013-2014. Liverpool ambao ni mabingwa mara tatu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya watachuana na timu ambayo itatangazwa baadaye katika Uwanja wa Taifa wa Rajamangala jijini Bangkok Julai 28 mwaka huu. Mkurugenzi Mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre amesema mara ya kwanza timu hiyo kwenda huko ilikuwa ni mwaka 2001 na mpaka sasa wameshakwenda mara nne hiyo inaonyesha jinsi gani wanavyowajali mashabiki wao waliopo nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo inaaminika kuwa na mashabiki wapatao milioni 14 nchini Thailand na mara ya mwisho kwenda huko ilikuwa mwaka 2009. Mbali na kwenda nchini Thailand klabu hiyo pia imepanga kucheza mechi zingine za kujipima nguvu katika nchi za Australia na Indonesia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment