Wednesday, April 17, 2013

LEVERKUSEN KUWAPA RAHA MASHABIKI WAKE KWA KUBORESHA HUDUMA ZA MTANDAO.

KLABU ya Bayern Liverkusen ya Ujerumani ambayo ina mpango wa kurejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao imebainisha mpango wao wa kuongeza mfumo wa kisasa zaidi wa mawasiliano kwa ajili ya mashabiki wao. Mashabiki wengi ambao wamekuwa wakiingia uwanjani hapo wamekuwa wakikumbwa na tatizo mtandao hafifu pamoja na mawasiliano yasiyoridhisha kwa kushindwa kupokea barua pepe au ujumbe mfupi kutokana na mahitaji makubwa yanayokuwepo kwa muda huo. Lakini matatizo hayo ya mawasiliano yatakuja kuwa historia katika Uwanja wa BayArena kuanzia Julai kutokana na mpango wao wa kuongeza viunganishi zaidi ya 350 vya mtandao visivyotumia waya ili kuwawezesha mashabiki wapatao 20,000 kutumia huduma kwa wakati mmoja bila usumbufu wowote. Ofisa Mkuu wa Leverkusen, Wolfgang Holzhaeuser amesema mashabiki wa kipindi hiki wanatumia zaidi huduma za mitandao ili kuwasiliana na jamaa na marafiki pindi wawapo uwanjani hivyo wanataka kuwapa huduma bora na isiyokuwa na usumbufu kwasababu ni haki yao.

No comments:

Post a Comment