Wednesday, April 17, 2013

PETROV AWASHUKURU MASHABIKI KWA KUMUOMBEA.

NAHODHA wa zamani wa klabu ya Aston Villa, Stiliyan Petrov amebainisha kuwa bado anasafari ndefu mpaka kupona kutokana na ugonjwa wa kansa ya damu au Leukaemia baada ya kugundulika nao Machi mwaka jana na kukiri kuwa ana bahati kuwa hai mpaka wakati huo. Petrov alizungumzia uzoefu wake kutokana na matibabu anayopata kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huo na shukrani zake kwa mashabiki ambao wamekuwa wakionyesha kumkumbuka katika kila mechi za klabu yake. Petrov amesema wakati alipogundulika alikuwa akijua aina ya ugonjwa uliokuwa ukimkabili lakini alikuwa hajui ni matibabu gani ambayo angekuwa akipewa ili kuudhibiti. Lakini wakati ameanza matibabu alishangaa muda mrefu ambao amekuwa akitumia dawa mpaka kuna wakati anajiuliza lini atamaliza dawa hizo lakini kutokana na subira na msaaada mkubwa anaopatiwa kutoka kwa familia yake na marafiki amefanikiwa kuvuka hatua hiyo ngumu. Petrov ambaye ni raia wa Bulgaria amesema anajiona kama mwenye bahati kwani wagonjwa wengi wanaougua ugonjwa huo kama yeye wanakufa haraka lakini yeye amefanikiwa kupambana mpaka hapo alipo. 

No comments:

Post a Comment