
Thursday, April 18, 2013
DROGBA ABURUZWA MAHAKAMANI.
KAMPUNI ya ujenzi ya kifaransa yenye maskani yake katika mji wa Ajaccio imemfungulia kesi mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba kwa tuhuma za kushindwa kulipa fedha zilizobakia za ujenzi wa nyumba yake. Mmiliki wa kampuni hiyo inayoitwa Acqua Viva, Leonard Simoni anadai kiasi cha euro 394,000 kama malipo yake ya kawaida na nyongeza ya euro 660,000 kama fidia na kesi hiyo imeanza kusikilizwa jana. Drogba na mkewe waliipa tenda kampuni hiyo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yao iliyoko jijini Abidjan lakini kampuni hiyo imedai kuwa wawili hao bado hawajalipa gharama za kazi za ziada zilizofanyika katika eneo hilo. Wakili Franck Dymarsky ambaye anamuwakilisha mshambuliaji huyo anayekipiga katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki ndiye anayemtetea kisheria nyota huyo katika kesi hiyo. Drogba pia amekamilisha hospitali aliyoijenga kwa paundi milioni tatu jijini Abidjan ambayo amedai kuwa itatoa huduma ya upendeleo kwa gharama nafuu zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment