Sunday, April 21, 2013

MADRID, BARCA ZAUA HISPANIA.

BAO la dakika za lala salama la Cesc Fabregas, jana limeipa Barcelona ushindi wa 1-0 dhidi ya Levante siku ambayo Eric Abidal alicheza mechi yake ya kwanza kwa dakika zote tisini tangu afanyiwe upasuaji wa ini. Huku mfungaji tegemeo wa timu hiyo Lionel Messi akiwa nje kwa maumivu yake ya nyama za paja la kulia ili awe fiti kabisa kabla ya kumenyana na Bayern Munich katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa, safu ya ushambuliaji ya Barcelona ilikosa makali yake mbele ya Levante hadi Fabregas alipofunga dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho. Ushindi huo unaisogeza Barcelona karibu kabisa na ubingwa wa La Liga, sasa ikiwa inaongoza kwa pointi 13 zaidi zikiwa zimebaki raundi sita. Kwa upande wa mahasimu wao Real Madrid nao walishinda mchezo wao kwa mabao 3-1 dhidi ya Real Betis na kukwea mpaka nafasi ya pili mwa msimamo wa La Liga mabao ambayo yalifungwa na Karim Benzema ambaye alifunga mawili na Metsu Ozil.

No comments:

Post a Comment