BONDIA wa uzito wa juu wa Uingereza, Dereck Chisora amefanikiwa kumchakaza Hector Alfredo Avila katika raundi ya tisa likiwa ni pambano lake la kwanza toka alipopata kipigo kutoka kwa David Haye Julai mwaka jana. Chisora mwenye umri wa miaka 29 alikuwa akipigana pambano lake la kwanza toka aliporejeshewa leseni yake Machi mwaka huu baada ya leseni hiyo kuzuiwa kufuatia vurugu za nje ya ulingo alizofanya na Haye mapema mwaka huu. Akihojiwa mara baada ya kumpiga Avila ambaye ni raia wa Argentina Chisora amesema lilikuwa pambano gumu kwasababu mpinzani wake alikuwa amempania lakini anashukuru amemaliza kwa ushindi na anasubiri mpinzani mwingine. Chisora anasubiri pambano linguine dhidi ya bondia mwingine wa uzito wa juu wa Uingereza David Price ambaye kabla ya kupambana na Chisora atapigana na Tony Thompson katika pambano la marudiano Julai mwaka huu.
No comments:
Post a Comment