Sunday, April 21, 2013

BAYERN HAINA KIKOSI B - HEYNCKES.

MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Jupp Heynckes amejitapa baada ya kuona kikosi chake cha pili kikiisambaratisha Hannover kwa mabao 6-1 na kudai kuwa klabu hiyo haina kikosi B. Heynckes ambaye amewahi kuifundisha Real Madrid katika mchezo huo uliochezwa jana aliwapumzisha wachezaji wake nyota wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona wakiwemo Bastian Schweisteiger, Philipp Lahm na Javi Martinez. Pamoja na kuwapumzisha nyota hao lakini Bayern walionekana moto wa kuotea mbali baada ya kupata ushindi huo mnono wa ugenini. Kocha amesema anajivua wachezaji alionao kwani wameonyesha tena kwamba timu hii haina kikosi B kwa kucheza soka safi na la kuvutia.

No comments:

Post a Comment